
| Chaneta wapigia magoti wahisani | Send to a friend |
| Saturday, 28 August 2010 20:00 |
|
CHAMA cha Netiboli Tanzania, CHANETA, kimepongeza baadhi ya wadhamini waliojitokeza kuchangia timu hiyo inayojiandaa na mashindano ya kimataifa ya Afrika na kimedai bado kinahitaji hisani ya Watanzania kutokana na bajeti yao kuhitaji sh70milioni kuwezesha timu hiyo kusafiri. Baadhi ya wadau wameanza kujitokeza na kutoa michango yao kitu ambacho Chama hicho kimetoa pongezi kubwa huku kikiwataka wadhamini zaidi wanaopenda kuchangia mchezo huo kujitokeza. Katibu Mkuu wa Chama hicho, Rose Mkisi alisema wamefurahishwa na baadhi ya wadau ambao wameonyesha moyo wa kuwasaidia lakini amedai kutokana na bajeti yao kuwa kubwa. Alisema bajeti hiyo ya sh70milioni imejumuhisha gharama zote za timu pamoja na tiketi za kwenda na kurudi. "Kikubwa, kwanza nawapongeza wote waliosaidia kufika hapa na kama mnavyofahamu timu hii inatakiwa kuondoka Septemba 5 kwenda Afrika Kusini na mpaka sasa bado hatujakamilisha taratibu za safari," alisema Mkisi. Mkisi alisema timu kamili itatangazwa mwanzoni mwa wiki ijayo na itakuwa na wachezaji 12 watakaosafiri kwenda Afrika Kusini tayari kwa mashindano hayo yatakayoshirikisha mataifa zaidi ya 10 Afrika. |

Habari Mpya
Picha
Zenye Mvuto
- Nafasi za Kazi
- Muswada wa madini waitoa jasho serikali
- Links za wateja na washirika wetu
- Bi kizee asafari kilometa 50 kupinga hotuba ya JK, AMUONYA ASITUMIE MADARAKA YAKE VIBAYA
- Mishahara sekta binafsi Tucta yashtukia danganya toto
- Vigogo UVCCM wajiuzulu
- Mwinyi atetea ajira za wafanyakazi, ashauri utu uheshimiwe kudumisha Amani












