MwanzoContactsEmail
Home Jumapili Habari JK: Sasa nitamwamchia Pinda kuongoza serikali
BOOKMARK THIS PAGE
JK: Sasa nitamwamchia Pinda kuongoza serikali  Send to a friend
Saturday, 28 August 2010 19:53

Exuper Kachenje, Katavi
 
MGOMBEA urais kupitia Chama Cha Mapinduzi, Jakaya Kikwete amesema kuwa atamuachia majukumu ya serikali Waziri Mkuu Mizengo Pinda ili yeye apate nafasi ya kufanya kampeni zake kwa nguvu zaidi.

Akihutubia katika mkutano wa hadhara jana kwenye uwanja wa Kashaulili, Mpanda mkoani Katavi, Rais Kikwete  pia alimuomba Pinda ampigie debe ili yeye na wagombea wengine wa CCM washinde kwa kishindo.
Kikwete ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM taifa na rais wa Tanzania, alisema kwa kuwa Pinda tayari amepita ushindi bila kupingwa na shughuli za serikali zipo, basi itabidi aendelee na shughuli za serikali.
 
 “Mpanda Mashariki mmetoa mchango mkubwa kwa kupata Waziri mkuu wa serikali inayoahidi na kutekeleza ahadi zake. Mzee hongera kwa kupita bila kupingwa, wenzako sie bado, uendelee kutupigia debe nasi tupite kwani bado tuna kazi,” alisema Rais Kikwete na kuongeza:
“Pinda ametusaidia sana, katika uendeshaji wa serikali, juzi tu alikuwa Rwanda na Burundi. Hivi karibuni ataenda Ghana na Umoja wa Mataifa kutuwakilisha. Shughuli za serikali zipo huyu mzee (Pinda) atakuwa anaendesha na mimi nitafanya kampeni bila taabu”, alisema Kikwete.
 
Kikwete alisema kuwa ndani ya mwaka huu mkoa wa Katavi na Rukwa itapatiwa jenereta mpya mbili za umeme zitazozalisha megawati 2.5 za umeme ambapo pia alisema zaidi ya magari ya wagonjwa 400 ya matairi matatu ytasambazwa maeneo mbalimbali.
 
Akiwa mjini Sumbawanga Kikwete alisema uwanja wa ndege wa mjini humo utaanza kujengwa.
 

Add this page to your favorite Social Bookmarking websites
Reddit! Del.icio.us! Mixx! Free and Open Source Software News Google! Live! Facebook! StumbleUpon! TwitThis Joomla Free PHP
 

Add comment

Tumia jukwaa ili kutoa maoni ambayo yatasaidia kulijenga taifa letu. Kumbuka, maoni yako yatapitiwa kwanza kabla hayajarushwa hewani!!!!!!


Banner
  • Kupiga Kura

  • Jumapili


Ajali ya Meli ZnZ inatufundisha nini?