MwanzoContactsEmail
Home Michezo Michezo ya Kimataifa AC Milan kuwaaa Juve
BOOKMARK THIS PAGE
AC Milan kuwaaa Juve  Send to a friend
Saturday, 28 January 2012 09:20

MILAN, Italia
MABINGWA wa Ligi ya 'Serie A', AC Milan watashuka dimbani katika mchezo wa robo fainali ya Kombe la Italia dhidi ya Juventus baada ya katikati ya wiki hii kuichapa Lazio 3-0 katika uwanja wao wa nyumbani mabao 3-1.
Djibril Cisse aliwashangaza wageni kwa kufunga bao la kuongoza dakika tano baada ya kuanza mchezo, kabla ya Milan kuibuka na kutawala mchezo vipindi vyote.

Katika muda wa dakika nne, Milan walikwamisha wavuni mabao mawili kupitia Robinho na Seedorf, kabla ya mshambuliaji wa kimataifa wa Sweden, Zlatan kukamilisha ushindi kwa kufunga bao la tatu.

Mshambuliaji wa kimataifa wa Brazil, Robinho alifunga bao lake kwa shuti kali la karibu na lango baada ya dakika 15 tangu kuanza mchezo likiwa bao la kusawazisha, na kiungo Seedorf aliipeleka mbele Milan kwa kufunga bao la pili baada ya kumuadaa kipa Federico Marchetti na kupiga shuti lililokwenda wavuni.

Ibrahimovic alikamilisha ushindi kwa kufunga bao la tatu dakika sita kabla ya mchezo kumalizika.
Matokeo hayo yatazikutanisha Milan na Juve katika mechi ya nusu fainali Februari. Katika mechi nyingine ya hatua ya nusu fainali, Napoli itacheza na Siena.

Juventus waliichapa AS Roma mabao 3-0 Jumanne iliyopita, huku Napoli wakiwatupa nje ya mashindano waliokuwa mabingwa watetezi, Inter Milan kwa kuichapa mabao 2-0 na Siena wakiiondoa Chievo Verona kwa bao 1-0.


Add this page to your favorite Social Bookmarking websites
Reddit! Del.icio.us! Mixx! Free and Open Source Software News Google! Live! Facebook! StumbleUpon! TwitThis Joomla Free PHP
 

Add comment

Tumia jukwaa ili kutoa maoni ambayo yatasaidia kulijenga taifa letu. Kumbuka, maoni yako yatapitiwa kwanza kabla hayajarushwa hewani!!!!!!


Banner