
| 'Fainali' ya Maugo, Cheka leo | Send to a friend |
| Saturday, 28 January 2012 09:22 |
|
HAKUNA ubishi leo burudani ya mchezo wa ndondi itaelekeza macho mjini Morogoro kutakapokuwa na pambano la kukata na shoka kati ya mabondia waliowahi kutwaa taji la Dunia IBF, Francis 'SMG' Cheka na Karama Nyilawila aliyetwaa taji la WBF. Mahasimu hao wanamaliza tambo na mbwembwe za maneno zilizodumu kwa wiki kadhaa kabla ya pambano lao la leo, raundi 10, uzito wa kilo 75. Kamisheni ya ngumi za kulipwa Tanzania (TPBC) imetoa baraka kufanyika pambano hilo. Awali lilikutana na changamoto za kutofanyika kufuatia Chama cha PST kugoma kutoa kibali kwa Nyilawila kucheza pambano hilo wakati akikabiliwa na pambano lingine la ubingwa wa WBF. Kufuatia hali hiyo, Nyilawila alikubali kuvuliwa ubingwa huo wa dunia ili aweze kuzichapa na Cheka katika pambano lisilo na ubingwa. Cheka ana rekodi ya kushinda mapambano 23 (13 kwa KO), amepigwa mara 6 (3 KO) na kutoka sare mara moja katika miaka 11. Cheka ana kila sababu ya kujivunia rekodi nzuri anapocheza Morogoro ambapo ameweza kushinda mfululizo dhidi ya Mada Maugo na Japhet Kaseba. Mpinzani wake ana rekodi ya kushinda mapambano 13 (6 KO)kapigwa mara 7 (3 KO) na sare 2 katika miaka mitano. Dhidi ya Cheka, litakuwa pambano lake la kwanza tangu atwae ubingwa wa WBF mwaka 2009. Kabla ya pambano hilo, kutakuwa na kisindikizo cha burudani kati ya mabondia wa Dar es Salaam watakaozikunja na mabondia wa Morogoro. |













