
| Serikali yagomea uwanja mpya | Send to a friend |
| Thursday, 02 September 2010 21:43 |
|
KIKAO cha siku nne kati ya serikali, Shirikisho la Soka Tanzania, TFF, Yanga na Simba juu ya kutumia Uwanja wa Taifa baada ya Uwanja wa Uhuru kufungwa, kimevunjika. Habari ambazo Mwananchi ilizipata jana jioni, zilisema kuwa mwafka umeshindwa kupatikana hasa baada ya Simba, Azam nao kutaka kutumia uwanja mpya baadaya Yanga kuanza kutuma maombi yao. Simba, Yanga, Azam , African Lyon na JKT Ruvu zilitakiwa kutafuta viwanja vya kutumia baada ya Uwanja wa Uhuru kufungwa kwa ajili ya marekebisho tayari kwa zoezi la kumwapisha rais baada ya uchaguzi wa Oktoba 30. Msemaji wa Yanga, Luis Sendeu alisema kikao kilichofanyika jana katika ofisi za Shirikisho la Soka Tanzania ( TFF), na kikiongozwa Leonard Thadeo kilishindwa kutoa majibu mazuri. Sendeu alisema kuwa awali wao ndio walikuwa wakwanza kuomba Serikali kutumia uwanja wa Taifa baada ya Serikali kuruhusu kuutumia uwanja huo huku watani wao wa jadi Simba wakiwa wanaenda Mwanza na Azam Tanga. Alisema cha ajabu baadaye Simba waliotangaza kuhamia Mwanza na Azam nazo zikabadilika na kuomba kuutumia uwanja huo kitu ambacho kilileta mvutano mkubwa hata. Kutokana na hali hiyo, Yanga ambayo awali ilipanga kutumia Uwanja wa Jamhuri, Morogoro na CCM Kirumba Mwanza, sasa kama kutakuwa na maamuzi mengine, yataamuliwa na Kamati ya Utendaji ya klabu itakayokutana leo. Kwa upande wa Simba Makamu Mwenyekiti wa klabu hiyo, Godfrey Nyange 'Kaburu' alisema kuwa baada ya serikali kusema hivyo wao watakwenda Mwanza kama walivyotangaza ila watawaaga mashabiki wao wa Dar es Salaam kwa mechi yao kirafiki na Gor Mahia ya Kenya. Alisema baada ya hapo watakwenda Tanga kwa ajili ya mechi yao ya Ligi Kuu kucheza na Azam kisha wataelekea Mwanza. |













