MwanzoContactsEmail
Home Michezo Kandanda Walioachwa Yanga wadai sh243mil
BOOKMARK THIS PAGE
Walioachwa Yanga wadai sh243mil  Send to a friend
Thursday, 02 September 2010 21:41

Sweetbert Lukonge

UONGOZI wa Chama cha Wachezaji Soka Tanzania (Sputanza) umelitaka Shirikisho la Soka Tanzania TFF kuhakikisha linasimamia kikamilifu madai ya wachezaji waliochwa na klabu ya Yanga ikiwa ni pamoja na timu hiyo kuwalipa mapema madai yao.

Kwa mujibu wa Sputanza wachezaji hao wanaidai klabu ya Yanga zaidi ya shilingi milioni 252.

Katibu mkuu wa Suptanza, Said George alisema kuwa klabu ya Yanga ilivunja mkataba na wachezaji hao ambao ni John Njoroge (Kenya) Wisdom Ndhlovu (Malawi) Ally Msigwa pamoja na Steven Malashi aliokuwa na mkataba wa kuitumika timu hiyo hadi 2012.

"Yanga wamekiuka mkataba na wanatakiwa kuwalipa wachezaji hao haki zao kwa kukiuka taratibu za mkataba...wawalipe mshahara kwa kipindi chote cha miaka iliyokuwa imebakia kabla ya kumalizika kwa mikataba yao, posho kwa ajili ya nauli, fedha za usajili za msimu wa 2009- 2010 walizokuwa wakiidai klabu hiyo," alisema George.

Alisema Malashi anaidai klabu hiyo jumla ya Sh 37,500,000 wakati  Ndhlovu sh 82,000,000 na Ally Msigwa sh 89,700,000. Njoroge anaidia klabu hiyo sh 44,000,000.

Alisema kutoka na hali ya kuvunjwa kwa mikataba ya wachezaji hao kulikofanya na viongozi wa Yanga bila ya kuheshim mikataba hiyo, klabu hiyo inatakiwa kuhakikisha inawalipa wachezaji hao madai yao na tayari uongozi wa Sputanza imeiandia TFF barua ya kuhakikisha inalisimamia sula hilo na wachezaji hao wanapata haki zao mapema iwezakanavyo.

Hata hivyo msemaji wa klabu ya Yanga Luis Sendeu alisema kuwa hawezi kulizunguzia suala hilo kwa sasa mpaka hapo suala hilo litakapo kuwa limejadiliwa na uongozi wa klabu hiyo.


Add this page to your favorite Social Bookmarking websites
Reddit! Del.icio.us! Mixx! Free and Open Source Software News Google! Live! Facebook! StumbleUpon! TwitThis Joomla Free PHP
 

Add comment

Tumia jukwaa ili kutoa maoni ambayo yatasaidia kulijenga taifa letu. Kumbuka, maoni yako yatapitiwa kwanza kabla hayajarushwa hewani!!!!!!


Banner