MwanzoContactsEmail
Home Habari Habari za Siasa Waziri Ngeleja awataka wabunge kufuata taratibu
BOOKMARK THIS PAGE
Waziri Ngeleja awataka wabunge kufuata taratibu  Send to a friend
Saturday, 28 January 2012 09:13

Mwandishi Wetu
WAZIRI wa Nishati na Madini, William Ngeleja, amewajia juu wabunge kuwa ugeni wa baadhi yao, isiwe utetezi wa kutofuata taratibu za mawasiliano kati ya Bunge na Serikali.

“Ugeni wa baadhi ya wabunge siyo utetezi wa kutofahamu taratibu za Bunge, kwa sababu Bunge ni taasisi. Tulishakubaliana taratibu za kupata mikataba ya Serikali na wawekezaji wanafahamu!” alisema Ngeleja.
Ngeleja alikuwa akizungumzia taarifa kuwa juzi alitimuliwa na Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini, baada ya kushindwa kuwasilisha sera na mikataba inayofafanua jinsi Watanzani watakavyonufaika na ushimbaji wa madini ya Uranium na athari zake.

Alisema lengo la kikao hicho lilikuwa ni kutoa taarifa ya utafutaji madini ya Uranium na kukutana na kampuni za utafutaji madini ya Uranium za Uranex na Mantra, hakuna sehemu iliyokuwa ikihusiana na uwasilishaji mikataba.
Waziri Ngeleja alisema suala la mikataba baina ya Serikali na wawekezaji siyo geni, lilishatolewa ufafanuzi mara nyingi na wabunge wanafahamu taratibu za kufuata ili kupata mikataba hiyo na kwamba, siyo kumlazimisha waziri kuzivunja kwa shinikizo.

“Utaratibu tuliokubaliana kati ya Serikali na Bunge ni kwamba, wakihitaji mkataba wowote, Katibu wa Bunge ataomba kwa maandishi serikalini na tutampelekea, watasambaziwa na watausoma kwa utaratibu maalumu,” alisema Ngeleja na kuongeza:

“Mpaka sasa ninavyozungumza Bunge halijaomba mikataba hiyo. Hata sisi Serikali tulishangazwa na hali ya jana, ingawa hatukufukuzwa kwa sababu tulizungumza tukaelewana na kukubaliana baadhi ya mambo.”
Aliendelea kuwa baada ya kuwakumbusha taratibu wanazotakiwa kufuata ili kupata mikataba hiyo, kikao hicho kilichokuwa chini ya uenyekiti wa Diana Chilolo, walishauri Serikali kuwapa semina na kujadili sera na madini ya madini na wasome kwanza mikataba hiyo.

“Tutawapa semina maalumu. Sasa tumetimliwa vipi? Serikali inasisitiza kamati iendelee kufuata utaratibu uliowekwa kupata mikataba siyo vinginevyo,” alisema Ngeleja.Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini, Januari Makamba, alinukuliwa juzi akisema kuwa walimfukuza waziri na maofisa wake kwa sababu hawawezi kujadili suala la madini ya Uranium bila kujua mpango ulioandaliwa na Serikali.

Hata hivyo, Ngeleja alisema wakati wa majadiliano na kamati hiyo, Makamba hakuwamo na kushangazwa na taarifa hizo.

Add this page to your favorite Social Bookmarking websites
Reddit! Del.icio.us! Mixx! Free and Open Source Software News Google! Live! Facebook! StumbleUpon! TwitThis Joomla Free PHP
 

Add comment

Tumia jukwaa ili kutoa maoni ambayo yatasaidia kulijenga taifa letu. Kumbuka, maoni yako yatapitiwa kwanza kabla hayajarushwa hewani!!!!!!


Banner
  • Kupiga Kura

  • Jumapili


Ajali ya Meli ZnZ inatufundisha nini?