MwanzoContactsEmail
Home Biashara Biashara za Kimataifa Wafanyakazi Afrika Kusini waitunishia misuli Serikali
BOOKMARK THIS PAGE
Wafanyakazi Afrika Kusini waitunishia misuli Serikali  Send to a friend
Thursday, 02 September 2010 22:06

JOHANNESBURG, Afrika Kusini

MGOMO wa wiki tatu wa wafanyakazi wa Umma nchini Afrika Kusini, sasa utaendelea kwa muda usiojulikana, baada ya Chama cha muungano wa vyama vya wafanyakazi nchini humo COSATU, kukataa nyongeza ya asilimia 7.5 iliyotolewa na serikali.

Katibu mkuu wa COSATU, Zwelinzima Vavi, amesema viongozi wengi wa vyama vya wafanyakazi ambao ni wanachama wake walipiga kura kukata nyogesa hiyo iliyotolewa na serikali.

Hata hivyo COSATU inasema vyama vingine vidogo vidogo vimetofautiana kuhusu nyingesa hiyo.
Mazungumzo zaidi ya kujaribu, kumaliza mgomo huo yanatarajiwa kuanza upya baadaye hii leo.
Serikali ya Afrika Kusini imetoa nyongesa ya asilimia 7.5 lakini wafanyakazi hao wanataka nyongesa ya asilimia 8.6.
BBC

Add this page to your favorite Social Bookmarking websites
Reddit! Del.icio.us! Mixx! Free and Open Source Software News Google! Live! Facebook! StumbleUpon! TwitThis Joomla Free PHP
 

Add comment

Tumia jukwaa ili kutoa maoni ambayo yatasaidia kulijenga taifa letu. Kumbuka, maoni yako yatapitiwa kwanza kabla hayajarushwa hewani!!!!!!


Banner