|
Meya Ilala atishia kusimamisha ujenzi wa Zahanati |
Send to a friend |
|
Saturday, 28 January 2012 09:00 |
|
Aziza Masoud MEYA wa Manispaa wa Ilala, Jerry Slaa amempa siku moja mkandarasi wa Kata ya Kipawa kuwasilisha hati na nyaraka zinazohusu mradi wa Zahanati ya kata hiyo pamoja na mchanganuo wa gharama zitazotumika kukamilisha mradi huo.
Slaa pia ametishia kusimamaisha ujenzi wa mradi huo kwa madai kuwa mkandarasi aliyepewa kazi hiyo kutokakuwa makini na kazi yake.
Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Slaa alisema ujenzi usiozingatia taratibu, na kutokuweka bango linaloonyesha kutekelezwa kwa mradi huo ni cha kihuni hali aliyosema inaweza kusababisha wananchi wa eneo husika kukosa imani na Serikali yao.
“Mradi huu sio wangu wala wa mkandarasi, huu ni mradi wa Wananchi sasa huu unaofanyika hapa ni ubabaishaji na kwa kuwa muda upo tuna uwezo hata wa kusimamisha mradi huu popote mtakapofikia kwa kuwataka mbomoe muanze upya kwa viwango tunavyovihitaji na vinavyoendana na fedha iliyotolewa,”alisema Slaa.
Alisema haiwezekani mkandarasi aliyepewa pesa za kutosha kufanya ujenzi usiozingatia taratibu za kitaalamu jambo alilosema linaweza kusababisha wananchi kukosa imani na viongozi wa eneo husika na kudhani fedha zilizotolewa zinaliwa na viongozi.
Alisema kuwa ni jukumu la viongozi kuhakikisha fedha zinazotolewa kwa ajili ya mradi zinaendana na mradi husika kwa kiwango cha ujenzi na ubora wa vifaa vinavyotumika kujengea jengo au mradi husika. “Hapa nataka nikija tena nimkute msimamizi na mkandarasi, kazi haiwezi ikajiendesha yenyewe na umwambie mwenyekiti afuatilie likizo kwa simu sio kwenda makao makuu kila siku na kuacha ofisi bila kiongozi,”alisema Slaa akitoa maagizo. Mwisho.
|